Zaburi 50:16-23
50:16 Za 25:10; Isa 29:13Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema:
“Una haki gani kunena sheria zangu
au kuchukua agano langu midomoni mwako?
50:17 1Fal 14:9; Mit 1:22; 5:12, 13; Rum 2:21; 2The 2:10-12Unachukia mafundisho yangu
na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
50:18 Rum 1:32; 1Tim 5:22; Ay 22:15Unapomwona mwizi, unaungana naye,
unapiga kura yako pamoja na wazinzi.
50:19 Za 10:7; 36:3; 52:2; 101:7Unakitumia kinywa chako kwa mabaya
na kuuongoza ulimi wako kwa hila.
50:20 Mt 10:21Wanena daima dhidi ya ndugu yako
na kumsingizia mwana wa mama yako.
50:21 Isa 57:11, 16; 62:1; 42:14; 64:12; 50:2; Mhu 8:11; Za 6:1; 18:15; 85:5; 76:6; 104:7; Rum 2:4Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya,
ukafikiri Mimi nami ni kama wewe.
Lakini nitakukemea
na kuweka mashtaka mbele yako.
50:22 Ay 8:13; Mik 5:8; Isa 17:10; Kum 32:39“Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu,
ama sivyo nitawararua vipande vipande,
wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa:
50:23 Za 85:13; 98:3; 9:14; 91:16; Isa 52:10Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi,
naye aiandaa njia yake
ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.”