Zaburi 35:11-18
35:11 Kut 23:1; Mt 26:60Mashahidi wakatili wanainuka,
wananiuliza mambo nisiyoyajua.
35:12 Yer 18:20; Za 38:20; 109:5; Mit 17:13Wananilipa baya kwa jema
na kuiacha nafsi yangu ukiwa.
35:13 2Sam 3:31; 1Fal 20:31; Za 30:11; 69:10, 11; 109:24; Ay 30:25Lakini walipokuwa wagonjwa, nilivaa nguo ya gunia
na nikajinyenyekesha kwa kufunga.
Maombi yangu yaliponirudia bila kujibiwa,
35:14 Za 38:6; 42:9; 43:2niliendelea kuomboleza
kama vile wao ni rafiki au ndugu.
Niliinamisha kichwa chini kwa huzuni
kama ninayemwombolezea mama yangu.
35:15 Ay 31:29; 16:10Lakini nilipojikwaa,
walikusanyika kwa shangwe;
washambuliaji walijikusanya dhidi yangu
bila mimi kujua.
Walinisingizia pasipo kukoma.
35:16 Za 22:7; Mk 10:34; 9:18; Ay 16:9; Mdo 7:54Kama watu wasiomcha Mungu, wamenidhihaki,
wamenisagia meno.
35:17 Za 6:3; 22:20, 21; 57:4; 58:6Ee Bwana, utatazama mpaka lini?
Niokoe maisha yangu na maangamizi yao,
uhai wangu wa thamani
kutokana na simba hawa.
35:18 Za 22:20, 25; 42:4; 109:30Nami nitakushukuru mbele ya kusanyiko kubwa,
nitakusifu katikati ya watu wengi.