Zaburi 18:16-24
18:16 Kut 15:5; Mit 18:4; 20:5; Za 69:2; 144:7Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;
alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
18:17 Za 38:19; 59:1; 143:9; Amu 18:26Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,
kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
18:18 Mit 1:27; 16:4; Yer 17:17; 40:2; Oba 1:13; Za 20:2; Isa 3:1Walinikabili siku ya msiba wangu,
lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
18:19 Za 31:8; 118:5; Hes 14:8Alinileta nje mahali penye nafasi tele,
akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
18:20 1Sam 22:21; 26:23; Ay 22:30; Za 24:4; Rum 2:12; 2Nya 15:7; 1Kor 3:8; Mit 6:4Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
18:21 2Nya 34:33; Za 37:34; 119:2; 102; Mit 8:32; 23:26Kwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
18:22 Za 119:30Sheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.
18:23 Mwa 6:9Nimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.
18:24 1Sam 26:23; Rut 2:12; Mt 10:41-42Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.