Zaburi 147:1-11
Zaburi 147
Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote
147:1 Za 135:3; 33:1Msifuni Bwana.
Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,
jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!
147:2 Za 51:18; 106:47; Kum 30:3; Isa 27:13; Yer 32:37; Eze 36:24Bwana hujenga Yerusalemu,
huwakusanya Israeli walio uhamishoni.
147:3 Za 34:18; Isa 1:6; 61:1; Eze 34:16; Ebr 12:13; Ay 5:18; Lk 4:18Anawaponya waliovunjika mioyo
na kuvifunga vidonda vyao.
147:4 Mwa 15:5; Isa 40:26Huzihesabu nyota
na huipa kila moja jina lake.
147:5 Kut 14:31; Nah 1:3; 1Nya 16:25; Za 48:1; 145:3; Isa 40:28Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,
ufahamu wake hauna kikomo.
147:6 2Nya 33:23; Za 146:8, 9; 37:9, 10; 145:20Bwana huwahifadhi wanyenyekevu
lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.
147:7 Za 30:4; 33:3; 42:4; 27:6; 98:5; Efe 2:20Mwimbieni Bwana kwa shukrani,
mpigieni Mungu wetu kinubi.
147:8 Kum 32:2; 11:14; 2Sam 1:21; Ay 26:8; 38:26; 5:10; 28:26; Za 104:14Yeye huzifunika anga kwa mawingu,
huinyeshea ardhi mvua,
na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.
147:9 Ay 38:41; Mt 6:26; Mwa 8:7; 1:30; Lk 12:24; Za 104:27, 28Huwapa chakula mifugo
na pia makinda ya kunguru yanapolia.
147:10 1Sam 16:7; Hos 1:7; Ay 39:11; Za 33:16-17Furaha yake haipo katika nguvu za farasi,
wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu.
147:11 Za 35:27; 33:18; 103:11; 119:43; 6:4Bwana hupendezwa na wale wamchao,
wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma.