Zaburi 119:9-16
Kutii Sheria Ya Bwana
119:9 Za 119:65, 169; 39:1; Mit 1:4, 10Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
119:10 Za 119:21, 118; 9:1; 2Nya 15:15Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
119:11 Isa 63:13; Mit 3:23; Za 119:133, 165; 18:22-23; Kum 6:6; Lk 2:19; Ay 22:22Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
119:12 Isa 63:13; Lk 2:19Sifa ni zako, Ee Bwana,
nifundishe maagizo yako.
119:13 Za 119:72Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote
zinazotoka katika kinywa chako.
119:14 Za 119:111Ninafurahia kufuata sheria zako
kama mtu afurahiaye mali nyingi.
119:15 Za 119:97, 148; 1:2Ninatafakari maagizo yako
na kuziangalia njia zako.
119:16 Za 112:1Ninafurahia maagizo yako,
wala sitalipuuza neno lako.