Zaburi 105:12-22
105:12 Kum 7:7; Ebr 11:9; Mwa 17:8; 23:4; 34:30Walipokuwa wachache kwa idadi,
wachache sana na wageni ndani yake,
105:13 Mwa 15:13-16; Hes 32:13; 33:3-49walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
105:14 Mwa 35:5; 12:17-20; 20:3; Za 9:5Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;
kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
105:15 Mwa 26:11; 20:7; 1Sam 12:3“Msiwaguse niliowatia mafuta;
msiwadhuru manabii wangu.”
105:16 Isa 3:1; Law 26:26; Mwa 12:10; 41:54; 2Fal 8:1; Eze 4:16Akaiita njaa juu ya nchi
na kuharibu chakula chao chote,
105:17 Mwa 45:5; 37:28; Mdo 7:9naye akatuma mtu mbele yao,
Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.
105:18 Mwa 40:15Walichubua miguu yake kwa minyororo,
shingo yake ilifungwa kwa chuma,
105:19 Mwa 12:10; 41:40; 40:20-21hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia,
hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.
105:20 Mwa 41:14Mfalme alituma watu wakamfungua,
mtawala wa watu alimwachia huru.
Alimfanya mkuu wa nyumba yake,
mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo,
105:22 Mwa 41:43-44; 41:40kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo
na kuwafundisha wazee wake hekima.