Mithali 9:13-18 NEN

Mithali 9:13-18

9:13 Mit 7:11; 5:6Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele;

hana adabu na hana maarifa.

9:14 Eze 16:25Huketi kwenye mlango wa nyumba yake,

juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,

9:15 Mit 1:20akiita wale wapitao karibu,

waendao moja kwa moja kwenye njia yao.

9:16 Mit 1:22Anawaambia wale wasio na akili,

“Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!”

9:17 Mit 20:17“Maji yaliyoibiwa ni matamu;

chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”

9:18 Mit 2:18; 7:26-27Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo,

kwamba wageni wake huyo mwanamke

wako katika vilindi vya kuzimu.

Read More of Mithali 9