Mithali 8:22-31 NEN

Mithali 8:22-31

8:22 Mit 3:19; Yn 1:1Bwana aliniumba mwanzoni mwa kazi yake,

kabla ya matendo yake ya zamani;

8:23 Mwa 1:26; Za 2:6; Mik 5:2; Yn 17:24niliteuliwa tangu milele,

tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.

8:24 Mwa 7:11Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa,

wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;

8:25 Ay 15:7kabla milima haijawekwa mahali pake,

kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,

8:26 Za 90:2kabla hajaumba dunia wala mashamba yake

au vumbi lolote la dunia.

8:27 Ay 26:7; Mit 3:19Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake,

wakati alichora mstari wa upeo wa macho

juu ya uso wa kilindi,

8:28 Ay 36:29; Mwa 1:7; Ay 9:8; 26:10wakati aliweka mawingu juu

na kuziweka imara chemchemi za bahari,

8:29 Ay 38:8-10; 1Sam 2:8wakati aliiwekea bahari mpaka wake

ili maji yasivunje agizo lake,

na wakati aliweka misingi ya dunia.

Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake.

Nilijazwa na furaha siku baada ya siku,

nikifurahi daima mbele zake,

8:31 Ay 28:25-27; Yn 1:1-4nikifurahi katika dunia yake yote

nami nikiwafurahia wanadamu.

Read More of Mithali 8