Mithali 8:1-11
Wito Wa Hekima
8:1 Mit 1:20; 9:3; Ay 28:12; 1Kor 1:24Je, hekima haitani?
Je, ufahamu hapazi sauti?
Juu ya miinuko karibu na njia,
penye njia panda, ndipo asimamapo;
8:3 Ay 29:7; Mit 7:6-13kando ya malango yaelekeayo mjini,
kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:
8:4 Isa 42:2“Ni ninyi wanaume, ninaowaita;
ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.
8:5 Mit 1:22; 1:4Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili;
ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.
8:6 Za 49:3; Mt 2:6, 7; Kol 1:26Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema;
ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa.
8:7 Za 37:30; Yn 8:14; Rum 15:8Kinywa changu husema lililo kweli,
kwa maana midomo yangu huchukia uovu.
Maneno yote ya kinywa changu ni haki;
hakuna mojawapo lililopotoka wala ukaidi.
Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi;
hayana kasoro kwa wale wenye maarifa.
8:10 Za 19:10; Mit 3:14-15Chagua mafundisho yangu badala ya fedha,
maarifa badala ya dhahabu safi,
8:11 Ay 28:15-19; Mit 3:13-15kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani
na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.