Mithali 7:6-20 NEN

Mithali 7:6-20

Kwenye dirisha la nyumba yangu

nilitazama nje kupitia upenyo

kwenye mwimo wa dirisha.

7:7 Mit 6:32Niliona miongoni mwa wajinga,

nikagundua miongoni mwa wanaume vijana,

kijana asiye na akili.

Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake,

akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke

7:9 Ay 24:15wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake,

giza la usiku lilipokuwa likiingia.

7:10 1Tim 2:9Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,

hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.

7:11 Mit 9:13; 1Tim 5:13(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,

miguu yake haitulii nyumbani;

7:12 Mit 8:1-36; 23:26-28mara kwenye barabara za mji,

mara kwenye viwanja vikubwa,

kwenye kila pembe huvizia.)

7:13 Mwa 39:12; Mit 1:20Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,

na kwa uso usio na haya akamwambia:

7:14 Law 7:11-18“Nina sadaka za amani nyumbani;

leo nimetimiza nadhiri zangu.

Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;

nimekutafuta na nimekupata!

7:16 Isa 19:9Nimetandika kitanda changu

kwa kitani za rangi kutoka Misri.

7:17 Amo 6:4; Mwa 37:25Nimetia manukato kitanda changu

kwa manemane, udi na mdalasini.

7:18 Mwa 39:7Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;

tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!

Mume wangu hayupo nyumbani;

amekwenda safari ya mbali.

Amechukua mkoba uliojazwa fedha

na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

Read More of Mithali 7