Mithali 7:21-27 NEN

Mithali 7:21-27

7:21 Mit 1:8-9; 8:32Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;

alimshawishi kwa maneno yake laini.

7:22 Ay 18:10Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke

kama fahali aendaye machinjoni,

kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,

7:23 Ay 15:22; 16:13; Mit 6:26; Mhu 9:12mpaka mshale umchome ini lake,

kama ndege anayenaswa kwenye mtego,

bila kujua itamgharimu maisha yake.

7:24 Mit 1:8-9; 8:32Sasa basi wanangu, nisikilizeni;

sikilizeni kwa makini nisemalo.

7:25 Mit 5:7-8Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,

wala usitangetange katika mapito yake.

7:26 Neh 13:26Aliowaangusha ni wengi;

aliowachinja ni kundi kubwa.

7:27 Amu 16:19; Ufu 22:15Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,7:27 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

Read More of Mithali 7