Mithali 6:12-19 NEN

Mithali 6:12-19

Mtu mbaya sana na mlaghai,

ambaye huzungukazunguka

na maneno ya upotovu,

6:13 Za 35:19; Mit 16:30ambaye anakonyeza kwa jicho lake,

anayetoa ishara kwa miguu yake

na kuashiria kwa vidole vyake,

6:14 Za 36:4; 140:2; Mik 2:1; Isa 32:7ambaye hupanga ubaya

kwa udanganyifu moyoni mwake:

daima huchochea fitina.

Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula;

ataangamizwa mara, pasipo msaada.

6:16 Mit 3:32; 8:13; 15:8, 9, 26; 16:5Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,

naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

6:17 Za 120:2; Mit 12:22; Yer 2:34; Mik 7:2; Hos 4:1-2macho ya kiburi,

ulimi udanganyao,

mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

6:18 Mwa 6:5; Ay 15:31; Rum 3:15moyo uwazao mipango miovu,

miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

6:19 Kum 19:16; Za 27:12; Mit 15:18; Zek 8:17shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,

na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

Read More of Mithali 6