Mithali 6:1-11 NEN

Mithali 6:1-11

Maonyo Dhidi Ya Upumbavu

6:1 Mwa 43:9; Ebr 7:22; Ezr 10:27; Mit 17:18Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,

ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi

kwa ajili ya mwingine,

kama umetegwa na ulichosema,

umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,

kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:

Nenda ukajinyenyekeshe kwake;

msihi jirani yako!

6:4 Rut 3:18; Za 132:4Usiruhusu usingizi machoni pako,

usiruhusu kope zako zisinzie.

6:5 Za 91:3; 2Sam 2:18; Isa 13:14; Za 91:3Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji,

kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.

6:6 Mit 6:11Ewe mvivu, mwendee mchwa;

zitafakari njia zake ukapate hekima!

Kwa maana yeye hana msimamizi,

wala mwangalizi, au mtawala,

6:8 Mit 30:24-25; 10:4lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi

na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

6:9 Mit 24:30-34; 26:13-16Ewe mvivu, utalala hata lini?

Utaamka lini kutoka usingizi wako?

6:10 Mit 24:33; Mhu 4:5Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

6:11 Mit 6:10-11; 20:13; 24:30-34hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

Read More of Mithali 6