Mithali 5:15-23 NEN

Mithali 5:15-23

Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe,

maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.

Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji

na vijito vyako vya maji viwanjani?

Na viwe vyako mwenyewe,

kamwe visishirikishwe wageni.

5:18 Wim 4:12-15; Kum 20:7; Mal 2:14Chemchemi yako na ibarikiwe

na umfurahie mke wa ujana wako.

5:19 Wim 2:9; 8:14Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri:

matiti yake na yakutosheleze siku zote,

nawe utekwe daima na upendo wake.

5:20 Mit 2:16; 7:5Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba?

Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?

5:21 Za 119:168; Hos 7:2; Yer 16:17; Ay 10:4; Ebr 4:13Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana,

naye huyapima mapito yake yote.

5:22 Za 9:16; Hes 32:23; Ay 18:9Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe;

kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.

5:23 Ay 4:21; 36:12Atakufa kwa kukosa nidhamu,

akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.

Read More of Mithali 5