Mithali 5:1-14 NEN

Mithali 5:1-14

Onyo Dhidi Ya Uzinzi

5:1 Mit 1:8Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu,

sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,

5:2 Mwa 2:7ili uweze kutunza busara

na midomo yako ihifadhi maarifa.

5:3 Za 55:21; Mit 2:16Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba

hudondoza asali,

na maneno ya kinywa chake

ni laini kuliko mafuta;

5:4 Mhu 7:26; Ebr 4:12lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,

mkali kama upanga ukatao kuwili.

5:5 Za 9:17; Mit 2:18Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;

hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.5:5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

5:6 Mit 9:13; 30:20Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima;

njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

5:7 Mit 1:8-9Sasa basi wanangu, nisikilizeni;

msiache ninalowaambia.

5:8 Mit 6:20-29; 7:1-27Njia zenu ziwe mbali naye,

msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine

na miaka yako kwa aliye mkatili,

5:10 Mit 29:3wageni wasije wakasherehekea utajiri wako

na jitihada yako ikatajirisha

nyumba ya mwanaume mwingine.

Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,

wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!

Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

Sikuwatii walimu wangu

wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

5:14 Mit 1:24-27; 6:33; 31:3Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa

katikati ya kusanyiko lote.”

Read More of Mithali 5