Mithali 4:1-9 NEN

Mithali 4:1-9

Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote

4:1 Mit 1:8; 19:20; Ay 8:10Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu;

sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu.

Ninawapa mafundisho ya maana,

kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu.

4:3 1Nya 29:1; 2Sam 12:24Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu,

ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu,

4:4 Mit 7:2; 1Nya 28:9baba alinifundisha akisema,

“Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;

yashike maagizo yangu na wewe utaishi.

4:5 Mit 3:13-18; 16:16Pata hekima, pata ufahamu;

usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.

4:6 2The 2:10; Mit 2:11Usimwache hekima naye atakuweka salama;

mpende, naye atakulinda.

4:7 Mt 13:44-46; Mit 23:23Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.

Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.

4:8 1Sam 2:30; Mit 3:18Mstahi, naye atakukweza;

mkumbatie, naye atakuheshimu.

4:9 Mit 1:8-9Atakuvika shada la neema kichwani mwako

na kukupa taji ya utukufu.”

Read More of Mithali 4