Mithali 31:10-20 NEN

Mithali 31:10-20

Maneno Ya Mwisho: Mke Mwenye Sifa Nzuri

31:10 Rut 3:11; Mit 19:14Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata?

Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani.31:10 Mithali 31:10-31 imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

31:11 Mwa 2:18; Mit 12:4Mume wake anamwamini kikamilifu

wala hakosi kitu chochote cha thamani.

Humtendea mumewe mema, wala si mabaya,

siku zote za maisha yake.

31:13 1Tim 2:9-10Huchagua sufu na kitani

naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii.

Yeye ni kama meli za biashara

akileta chakula chake kutoka mbali.

31:15 Mt 24:45; Rum 12:11; Ay 23:12Yeye huamka kungali bado giza

huwapa jamaa yake chakula

na mafungu kwa watumishi wake wa kike.

Huangalia shamba na kulinunua,

kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu.

Hufanya kazi zake kwa nguvu,

mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake.

Huona kwamba biashara yake ina faida,

wala taa yake haizimiki usiku.

Huweka mikono yake kwenye pia,

navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.

31:20 Kum 15:11; Ebr 13:16; Efe 4:26-28Huwanyooshea maskini mikono yake

na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

Read More of Mithali 31