Mithali 30:1-10 NEN

Mithali 30:1-10

Misemo Ya Aguri

30:1 Mit 22:17Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia:

Huyu mtu alimwambia Ithieli,

naam, kwa Ithieli na kwa Ukali:

30:2 Za 73:22“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote;

sina ufahamu wa kibinadamu.

30:3 Mit 9:10Sijajifunza hekima,

wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.

30:4 Kum 30:12; Ufu 19:12; Yn 3:13; Ay 26:8; Efe 4:7-10Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka?

Ni nani ameshakusanya upepo

kwenye vitanga vya mikono yake?

Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake?

Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia?

Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani?

Niambie kama unajua!

30:5 Za 18:30; 12:6; 84:11“Kila neno la Mungu ni kamilifu;

yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.

30:6 Kum 12:32; Ufu 22:18Usiongeze kwenye maneno yake,

ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.

“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana;

usininyime kabla sijafa:

30:8 Mt 6:18Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo;

usinipe umaskini wala utajiri,

bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.

30:9 Neh 9:25; Kum 6:12; 8:12; Yos 24:27; Hos 13:6Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana

na kusema, ‘Bwana ni nani?’

Au nisije nikawa maskini nikaiba,

nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.

“Usimchongee mtumishi kwa bwana wake,

asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo.

Read More of Mithali 30