Mithali 3:21-35 NEN

Mithali 3:21-35

3:21 Mit 1:8-9; 6:20; 4:20-22Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara,

usiache vitoke machoni pako;

3:22 Kum 30:20; Mit 4:20-22ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako

na pambo la neema shingoni mwako.

Kisha utaenda katika njia yako salama,

wala mguu wako hautajikwaa;

3:24 Law 26:6; Za 3:5; Ay 11:18; Yer 31:25ulalapo, hautaogopa;

ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.

3:25 Za 91:5; 112:7Usiogope maafa ya ghafula

au maangamizi yanayowapata waovu,

3:26 1Sam 2:9kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako

na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.

3:27 Rum 13:7; Gal 6:10Usizuie wema kwa wale wanaostahili

ikiwa katika uwezo wako kutenda.

3:28 Law 19:13; Lk 10:25-37; Kum 24:15Usimwambie jirani yako,

“Njoo baadaye, nitakupa kesho”:

wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.

3:29 Zek 8:17Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako,

ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini.

3:30 Rum 12:18Usimshtaki mtu bila sababu,

wakati hajakutenda dhara lolote.

3:31 Za 37:1; Mit 24:1-2Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri

wala kuchagua njia yake iwayo yote,

3:32 Za 101:4; Ay 29:4kwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu,

lakini siri yake iko kwa mwenye haki.

3:33 Ay 5:3; Mal 2:2; Zek 5:4Laana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu,

lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.

3:34 Za 18:25-27; Mt 23:12Huwadhihaki wale wanaodhihaki,

lakini huwapa neema wale wanyenyekevu.

Wenye hekima hurithi heshima,

bali huwaaibisha wapumbavu.

Read More of Mithali 3