Mithali 3:11-20 NEN

Mithali 3:11-20

3:11 Mit 1:8-9; Ay 5:17Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana

na usichukie kukaripiwa naye,

3:12 Mit 13:24; Ufu 3:19; Ay 3:19; 5:17; Ebr 12:5-6kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,

kama vile baba afanyavyo

kwa mwana apendezwaye naye.

3:13 Mit 8:34, 35Heri mtu yule aonaye hekima,

mtu yule apataye ufahamu,

3:14 Ay 28:15; Mit 16:16kwa maana hekima ana faida kuliko fedha

na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.

3:15 Ay 28:17-19Hekima ana thamani kuliko marijani;

hakuna chochote unachokitamani

kinachoweza kulinganishwa naye.

3:16 1Fal 3:13-14; Mit 8:18Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;

katika mkono wake wa kushoto

kuna utajiri na heshima.

3:17 Mit 16:7; Mt 11:28-30Njia zake zinapendeza,

mapito yake yote ni amani.

3:18 Mwa 2:9; Ufu 2:7Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;

wale wamshikao watabarikiwa.

3:19 Ay 28:25-27; Za 104:24; Mit 8:27-29Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia,

kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake;

3:20 Kum 33:28; Ay 36:28kwa maarifa yake vilindi viligawanywa,

nayo mawingu yanadondosha umande.

Read More of Mithali 3