Mithali 3:1-10 NEN

Mithali 3:1-10

Faida Nyingine Za Hekima

3:1 Kum 30:16; Za 44:17; Mit 4:5Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,

bali zitunze amri zangu moyoni mwako,

3:2 Mit 9:6; 4:10kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako

na kukuletea mafanikio.

3:3 Kum 6:8; Mit 6:21; 2Kor 3:3Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe;

vifunge shingoni mwako,

viandike katika ubao wa moyo wako.

3:4 1Sam 2:26; Lk 2:52; Mdo 2:47Ndipo utapata kibali na jina zuri

mbele za Mungu na mwanadamu.

3:5 Za 4:5; Yer 9:23Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote

wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

3:6 1Nya 28:9; Ay 33:11; Yer 42:3katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

3:7 Isa 5:21; Rum 12:16; Kum 4:6Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;

mche Bwana ukajiepushe na uovu.

3:8 Za 38:3; Mit 4:22; Ay 21:24Hii itakuletea afya mwilini mwako,

na mafuta kwenye mifupa yako.

3:9 Kut 23:19; 26:1-15Mheshimu Bwana kwa mali zako na

kwa malimbuko ya mazao yako yote;

3:10 Kum 28:8; Za 144:13; Ay 22:21; Mal 3:10-12ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika,

viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.

Read More of Mithali 3