Mithali 29:19-27 NEN

Mithali 29:19-27

Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu,

ajapoelewa, hataitikia.

29:20 Mit 14:17Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka?

Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.

Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani,

atamletea sikitiko mwishoni.

29:22 Mit 14:17Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi,

naye mtu mwenye hasira ya haraka

hutenda dhambi nyingi.

29:23 Isa 66:2; Mt 23:12; Yak 4:6Kiburi cha mtu humshusha,

bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu

hupata heshima.

29:24 Law 5:1Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe;

huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.

29:25 1Sam 15:24; Mit 28:25; 16:20Kuwaogopa watu huwa ni mtego,

bali yeyote amtumainiaye Bwana atakuwa salama.

29:26 Mit 19:6; 16:33Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala,

bali mtu hupata haki kutoka kwa Bwana.

29:27 Mit 29:10Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu;

waovu huwachukia sana wenye haki.

Read More of Mithali 29