Mithali 29:1-9
29:1 2Nya 36:16; Mit 6:15Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi,
ataangamia ghafula, wala hapati dawa.
29:2 2Fal 11:20; Es 8:15; Mit 28:12Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi;
waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
29:3 1Fal 1:48; Mit 10:1; 23:15-16; 5:8-10; Lk 15:11-32Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
29:4 Mit 8:15-16Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti,
bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
29:5 Ay 32:21; Mit 26:28Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili,
anautandaza wavu kuitega miguu yake.
29:6 Ay 5:13; Mhu 9:12Mtu mbaya hutegwa na dhambi yake mwenyewe
bali mwenye haki huweza kuimba na kufurahi.
29:7 Ay 29:16; Za 41:1; Isa 35:3-4Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini,
bali mwovu hajishughulishi na hilo.
29:8 Mit 11:11; 16:14Wenye mzaha huuchochea mji,
bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira.
29:9 Mt 11:17Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu,
mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.