Mithali 28:7-17 NEN

Mithali 28:7-17

28:7 Mit 23:19-21Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye ufahamu,

bali rafiki wa walafi humwaibisha baba yake.

28:8 Ay 27:16-17; Eze 18:8; Kut 18:21; Mit 13:22; Lk 14:12-14Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno

hukusanya kwa ajili ya mwingine,

ambaye atawahurumia maskini.

28:9 Za 66:18; Zek 7:11; Isa 1:13; 2Tim 4:3Kama mtu yeyote akikataa kusikia sheria,

hata maombi yake ni chukizo.

28:10 Za 34:9; 57:6; Mk 10:30; Mit 26:27; Rum 8:32Yeye ambaye humwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya,

ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe,

bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.

Mtu tajiri anaweza kuwa na hekima machoni pake mwenyewe,

bali mtu maskini mwenye ufahamu atamfichua.

28:12 2Fal 11:20; Ay 24:4; Mit 11:10Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa,

bali waovu watawalapo, watu hujificha.

28:13 1Yn 1:8-10; 2Sam 12:13; Ay 31:33; Dan 4:27Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa,

bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema.

28:14 Za 16:8; Mit 23:17; Rum 2:5; 11:20Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha Bwana,

bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu

huangukia kwenye taabu.

Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye,

ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge.

Mtawala dhalimu hana akili,

bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu

atafurahia maisha marefu.

28:17 Mwa 9:6; 1Sam 30:17Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua

atakuwa mtoro mpaka kufa;

mtu yeyote na asimsaidie.

Read More of Mithali 28