Mithali 28:18-28
28:18 Es 6:13; Mit 10:9Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama
hulindwa salama,
bali yeye ambaye njia zake ni potovu
ataanguka ghafula.
28:19 Mit 12:11Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,
bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha.
28:20 Mit 13:11; 20:21; 23:4, 22; 1Tim 6:9Mtu mwaminifu atabarikiwa sana,
bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka
hataacha kuadhibiwa.
28:21 Eze 13:19; Za 94:21; Mit 18:5Kuonyesha upendeleo si vizuri,
hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate.
28:22 Mit 28:20Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri,
naye hana habari kuwa umaskini unamngojea.
28:23 Mit 27:5, 6Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi,
kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili.
28:24 Mit 18:9; 19:26Yeye amwibiaye babaye au mamaye
na kusema, “Si kosa,”
yeye ni mwenzi wa yule aharibuye.
28:25 1Tim 6:6; Mit 29:25Mtu mwenye tamaa huchochea fitina,
bali yule amtegemeaye Bwana atafanikiwa.
28:26 Za 4:5; Mit 3:5Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu,
bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama.
28:27 Kum 15:7; Mit 19:17; 22:9Yeye ampaye maskini
hatapungukiwa na kitu chochote,
bali yeye awafumbiaye maskini macho
hupata laana nyingi.
28:28 Mit 28:12; Ay 20:19Wakati waovu watawalapo,
watu huenda mafichoni,
bali waovu wanapoangamia,
wenye haki hufanikiwa.