Mithali 27:5-14 NEN

Mithali 27:5-14

27:5 Gal 2:14Afadhali karipio la wazi

kuliko upendo uliofichika.

27:6 Za 141:5; Mit 28:23Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu,

bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

27:7 Ay 6:7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali,

bali kwa mwenye njaa

hata kile kilicho kichungu

kwake ni kitamu.

27:8 Isa 16:2; Ay 39:14Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake,

ndivyo alivyo mtu atangatangaye

mbali na nyumbani mwake.

27:9 Es 2:12; Za 45:8Manukato na uvumba huleta furaha moyoni,

nao uzuri wa rafiki huchipuka

kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.

27:10 Mit 17:17Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,

tena usiende nyumbani mwa ndugu yako

wakati umepatwa na maafa.

Bora jirani wa karibu

kuliko ndugu aliye mbali.

27:11 Mit 10:1; 23:15-16; Mwa 24:60Mwanangu, uwe na hekima,

nawe ulete furaha moyoni mwangu,

ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote

anitendaye kwa dharau.

27:12 Mit 22:3Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,

bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa.

27:13 Mit 20:16Chukua vazi la yule awekaye dhamana

kwa ajili ya mgeni;

lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo

kwa ajili ya mwanamke mpotovu.

27:14 Za 12:2Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu

asubuhi na mapema,

itahesabiwa kama ni laana.

Read More of Mithali 27