Mithali 27:23-27, Mithali 28:1-6 NEN

Mithali 27:23-27

27:23 Mit 12:10; Yer 5:3Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako

ya kondoo na mbuzi,

angalia kwa bidii ngʼombe zako.

27:24 Mit 23:5Kwa kuwa utajiri haudumu milele,

nayo taji haidumu vizazi vyote.

27:25 Za 104:14Wakati majani makavu yameondolewa

na mapya yamechipua,

nayo majani toka milimani yamekusanywa,

wana-kondoo watakupatia mavazi

na mbuzi thamani ya shamba.

Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi

kukulisha wewe na jamaa yako,

na kuwalisha watumishi wako wa kike.

Read More of Mithali 27

Mithali 28:1-6

28:1 2Fal 7:7; Law 26:17; Za 53:5Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza,

bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi,

bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu.

28:3 Mt 18:28Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi

ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao.

28:4 1Fal 18:18; Mt 3:7; Efe 5:11; 1Tim 5:20Wale waiachao sheria huwasifu waovu,

bali wale waishikao sheria huwapinga.

28:5 Yn 7:17; 1Kor 2:15Watu wabaya hawaelewi haki,

bali wale wamtafutao Bwana wanaielewa kikamilifu.

28:6 Mit 19:1Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama

kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.

Read More of Mithali 28