Mithali 27:15-22 NEN

Mithali 27:15-22

27:15 Es 1:18; Mit 19:13Mke mgomvi ni kama

matone yasiyokoma ya siku ya mvua.

Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo

au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.

Kama vile chuma kinoavyo chuma,

ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.

27:18 1Kor 9:7; Lk 19:12-27; Kum 20:6Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake,

naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.

Kama uso uonekanavyo kwenye maji,

ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.

27:20 Mit 30:15-16; Hab 2:5; Mhu 6:7Kuzimu na Uharibifu havishibi

kadhalika macho ya mwanadamu.

27:21 Mit 17:3Kalibu ni kwa ajili ya fedha

na tanuru kwa ajili ya dhahabu,

bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.

27:22 Isa 1:5; Yer 5:3; Mit 23:35Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,

ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,

hutauondoa upumbavu wake.

Read More of Mithali 27