Mithali 26:3-12 NEN

Mithali 26:3-12

26:3 Za 32:9; Mit 10:13Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda,

nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!

26:4 Isa 36:21Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake,

ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.

26:5 Mt 16:14; 21:24-27; Mit 3:7Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake,

ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.

26:6 Mit 10:26Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara,

ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.

26:7 Mit 26:9Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia

ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.

26:8 Mit 26:1Kama kufunga jiwe kwenye kombeo,

ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.

26:9 Mit 26:7Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi

ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu.

Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo,

ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.

26:11 Kut 8:15; Za 85:8; 2Pet 2:22Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake,

ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.

26:12 Ufu 3:17; Mit 29:20Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima

machoni pake mwenyewe?

Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.

Read More of Mithali 26