Mithali 25:21-28, Mithali 26:1-2 NEN

Mithali 25:21-28

25:21 Kut 23:4; Mt 5:44; Rum 12:20Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale;

kama ana kiu, mpe maji anywe.

25:22 2Sam 16:22; Mt 5:44; Za 18:8Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake,

naye Bwana atakupa thawabu.

25:23 Ay 37:22; Za 105:5Kama vile upepo wa kaskazini uletavyo mvua,

ndivyo ulimi usingiziao uletavyo uso wa hasira.

25:24 Mit 19:13; 21:9, 19Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,

kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

Kama vile maji baridi kwa nafsi iliyochoka

ndivyo zilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali.

25:26 Mik 7:8Kama vile chemchemi iliyotibuliwa matope au

kisima kilichotiwa taka

ndivyo alivyo mtu mwenye haki

akishiriki na waovu.

25:27 Mit 27:2; Mt 23:12; Lk 14:11Si vyema kula asali nyingi sana,

wala si heshima

kujitafutia heshima yako mwenyewe.

25:28 Mit 16:32Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka

ndivyo alivyo mtu

ambaye hawezi kujitawala mwenyewe.

Read More of Mithali 25

Mithali 26:1-2

26:1 Isa 32:6; 1Sam 12:17; Mit 19:10Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno,

ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.

26:2 Hes 23:8; Kum 23:5Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake

au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi,

ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.

Read More of Mithali 26