Mithali 25:1-10 NEN

Mithali 25:1-10

Mithali Zaidi Za Solomoni

25:1 1Fal 4:32Hizi ni mithali zaidi za Solomoni, zilizonakiliwa na watu wa Hezekia mfalme wa Yuda:

25:2 Kum 29:29; Rum 11:33; Mit 10:10-15Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo,

bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo.

Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini,

ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki.

25:4 2Tim 2:21Ondoa takataka kwenye madini ya fedha,

nako ndani yake kutatokea chombo

cha mfua fedha.

25:5 2Sam 7:13; Mit 20:8; 29:14Ondoa waovu mbele ya mfalme,

nacho kiti chake cha enzi

kitaimarishwa kwa njia ya haki.

Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme,

wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu;

25:7 Lk 14:7-10ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,”

kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu.

Kile ulichokiona kwa macho yako

25:8 Mit 17:14; Mt 5:25-26usiharakishe kukipeleka mahakamani,

maana utafanya nini mwishoni

kama jirani yako atakuaibisha?

25:9 Mt 5:25; 18:15Kama ukifanya shauri na jirani yako,

usisaliti siri ya mtu mwingine,

ama yeye aisikiaye aweza kukuaibisha

na kamwe sifa yako mbaya haitaondoka.

Read More of Mithali 25