Mithali 24:5-14
24:5 Mit 21:22Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa,
naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu,
24:6 Mit 11:14; Lk 14:31kwa kufanya vita unahitaji uongozi
na kwa ushindi washauri wengi.
24:7 Za 10:5; Mit 14:6Hekima i juu mno kwa mpumbavu,
katika kusanyiko langoni
hana lolote la kusema.
24:8 Rum 1:30Yeye apangaye mabaya
atajulikana kama mtu wa hila.
24:9 Mwa 6:5; Za 119:113; Mt 9:4; Mdo 8:22; 2Kor 10:524:9 Mwa 6:5; Mdo 8:22; 2Kor 10:5Mipango ya upumbavu ni dhambi,
watu huchukizwa na mwenye dhihaka.
24:10 Yer 51:46; Ebr 12:3Ukikata tamaa wakati wa taabu,
jinsi gani nguvu zako ni kidogo!
24:11 Isa 58:6-7; 1Yn 3:16; Za 82:4Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo;
wazuie wote wanaojikokota
kuelekea machinjoni.
24:12 Za 139:2; Mit 16:24; 21:2; Yer 32:19; Mt 16:24Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,”
je, yule apimaye mioyo halitambui hili?
Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili?
Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?
24:13 Wim 5:1Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri;
asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja.
24:14 Za 119:103; Mit 16:24; 23:18Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako,
kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,
nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.