Mithali 24:23-34 NEN

Mithali 24:23-34

Misemo Zaidi Ya Wenye Hekima

24:23 Kut 18:16; Law 19:15; 2Nya 19:7; Za 72:2; Yer 22:16; Yn 7:24Hii pia ni misemo ya wenye hekima:

Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema:

24:24 Isa 5:23; Mit 17:15Yeyote amwambiaye mwenye hatia,

“Wewe huna hatia,”

Kabila zitamlaani

na mataifa yatamkana.

Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia,

nazo baraka tele zitawajilia juu yao.

Jawabu la uaminifu

ni kama busu la midomoni.

24:27 1Fal 5:17, 18; Lk 14:28Maliza kazi zako za nje,

nawe uweke mashamba yako tayari,

baada ya hayo, jenga nyumba yako.

24:28 Za 7:4; Efe 4:25Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu,

au kutumia midomo yako kudanganya.

24:29 Mit 20:22; Rum 12:17; Mt 5:39Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi;

nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”

24:30 Mit 6:6-11; 26:13-16Nilipita karibu na shamba la mvivu,

karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,

24:31 Yer 4:3; Ebr 6:8miiba ilikuwa imeota kila mahali,

ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na

ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.

Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona,

nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:

24:33 Mit 6:10Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,

bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

24:34 Mit 10:4; Mhu 10:18hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,

na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.

Read More of Mithali 24