Mithali 24:15-22 NEN

Mithali 24:15-22

24:15 Za 10:9, 10Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia

makao ya mwenye haki,

wala usiyavamie makazi yake,

24:16 Ay 5:19; Mik 7:8; Za 34:19Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena,

lakini waovu huangushwa chini na maafa.

24:17 Oba 1:12; Ay 31:29Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo;

wakati ajikwaapo,

usiruhusu moyo wako ushangilie.

24:18 Ay 31:29Bwana asije akaona na kuchukia

akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.

24:19 Za 37:1Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya

wala usiwaonee wivu waovu,

24:20 Ay 18:5; Mit 13:9; Isa 3:11kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo,

nayo taa ya waovu itazimwa.

24:21 Rum 13:1-7; 1Pet 2:17Mwanangu, mche Bwana na mfalme,

wala usijiunge na waasi,

24:22 Za 73:19kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao,

naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?

Read More of Mithali 24