Mithali 23:29-35, Mithali 24:1-4 NEN

Mithali 23:29-35

23:29 1Fal 20:16; Mit 20:1; Isa 5:11; Nah 1:10; Mt 24:49, 50; Efe 5:18Ni nani mwenye ole?

Ni nani mwenye huzuni?

Ni nani mwenye ugomvi?

Ni nani mwenye malalamiko?

Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu?

Ni nani mwenye macho mekundu?

23:30 Za 75:8; Efe 5:18; Mit 20:1; Efe 5:18; Za 75:8; Mit 9:2Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo,

hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu,

wakati unapometameta kwenye bilauri,

wakati ushukapo taratibu!

Mwishowe huuma kama nyoka

na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

Macho yako yataona mambo mageni

na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka.

Utakuwa kama alalaye katikati ya bahari,

alalaye juu ya kamba ya merikebu.

23:35 Mit 27:22; Yer 5:3; Kum 29:19; Isa 56:12; 2Pet 2:22Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia!

Wamenichapa, lakini sisikii!

Nitaamka lini

ili nikanywe tena?”

Read More of Mithali 23

Mithali 24:1-4

24:1 Mit 3:31-32; 23:17-18Usiwaonee wivu watu waovu,

usitamani ushirika nao;

24:2 Za 2:1; 10:7; Isa 32:6; 55:7-8; 59:7; 65:2; Hos 4:1kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri,

nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara.

24:3 Mit 14:1Kwa hekima nyumba hujengwa,

nayo kwa njia ya ufahamu huimarishwa

24:4 Mit 8:21kwa njia ya maarifa vyumba vyake hujazwa

vitu vya thamani na vya kupendeza.

Read More of Mithali 24