Mithali 23:19-28 NEN

Mithali 23:19-28

23:19 Kum 4:9; Mit 28:7Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima,

weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa.

23:20 Hab 2:15; Rum 13:13; Isa 5:22Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo,

au wale walao nyama kwa pupa,

23:21 Mit 21:17; 19:23; 19:15kwa maana walevi na walafi huwa maskini,

nako kusinzia huwavika matambara.

23:22 Law 19:32; Efe 6:1-2Msikilize baba yako, aliyekuzaa,

wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.

23:23 Mit 4:7; 17:16; Mt 13:44Nunua kweli wala usiiuze,

pata hekima, adabu na ufahamu.

23:24 Mit 23:15-16; 10:1; 15:20Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,

naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

23:25 Mit 10:1Baba yako na mama yako na wafurahi,

mama aliyekuzaa na ashangilie!

23:26 Mit 5:1-6; Za 18:21Mwanangu, nipe moyo wako,

macho yako na yafuate njia zangu,

23:27 Mit 22:14kwa maana kahaba ni shimo refu

na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba.

23:28 Mit 7:11-12; Mhu 7:26Kama mnyangʼanyi, hungojea akivizia,

naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume.

Read More of Mithali 23