Mithali 23:10-18 NEN

Mithali 23:10-18

23:10 Kum 19:14; Mit 22:28Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani

wala kunyemelea kwenye mashamba ya yatima,

23:11 Ay 19:25; Kut 22:22-24; Yer 50:34; Mit 15:25kwa kuwa Mtetezi wao ni mwenye nguvu,

atalichukua shauri lao dhidi yako.

23:12 Mit 2:2Elekeza moyo wako kwenye mafundisho

na masikio yako kwenye maneno ya maarifa.

23:13 Mit 13:24; 19:18; 22:18; 22:15; 29:15, 16Usimnyime mtoto adhabu,

ukimwadhibu kwa fimbo, hatakufa.

23:14 Mit 13:24; 19:18Mwadhibu kwa fimbo

na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini.23:14 Mautini maana yake ni Kuzimu.

23:15 Mit 23:24, 25; 29:3Mwanangu, kama moyo wako una hekima,

basi moyo wangu utafurahi,

23:16 Mit 23:24utu wangu wa ndani utafurahi,

wakati midomo yako

itakapozungumza lililo sawa.

23:17 Za 73:3; Mit 28:14Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi,

bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Bwana.

23:18 Za 37:1-4; Mit 24:14-20Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako,

nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali.

Read More of Mithali 23