Mithali 22:28-29, Mithali 23:1-9 NEN

Mithali 22:28-29

22:28 Kum 19:14Usisogeze jiwe la mpaka wa zamani

lililowekwa na baba zako.

22:29 1Fal 11:28; Mwa 41:46; Mhu 9:10Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake?

Atahudumu mbele ya wafalme;

hatahudumu mbele ya watu duni.

Read More of Mithali 22

Mithali 23:1-9

Uketipo kula chakula na mtawala,

angalia vyema kile kilicho mbele yako,

na utie kisu kooni mwako

kama ukiwa mlafi.

23:3 Za 141:4Usitamani vyakula vyake vitamu

kwa kuwa chakula hicho ni cha hila.

23:4 Yn 6:27; 1Tim 6:9; Rum 12:16Usijitaabishe ili kuupata utajiri,

uwe na hekima kuonyesha kujizuia.

23:5 Mt 6:19; Mit 27:24Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka,

huwa kama umepata mabawa ghafula,

ukaruka na kutoweka angani kama tai.

23:6 Za 141:4; Kum 15:9Usile chakula cha mtu mchoyo,

usitamani vyakula vyake vitamu,

23:7 Za 12:2kwa maana yeye ni aina ya mtu

ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama.

Anakuambia, “Kula na kunywa,”

lakini moyo wake hauko pamoja nawe.

Utatapika kile kidogo ulichokula,

nawe utakuwa umepoteza bure

maneno yako ya kumsifu.

23:9 Mit 9:7Usizungumze na mpumbavu,

kwa maana atadhihaki hekima ya maneno yako.

Read More of Mithali 23