Mithali 22:17-27 NEN

Mithali 22:17-27

Misemo Ya Wenye Hekima

22:17 Mit 1:8; 1:6; 30:1; 31:1; 2:2Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima,

elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo,

kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako

na kuwa nayo yote tayari midomoni mwako.

Ili tumaini lako liwe katika Bwana,

hata wewe, ninakufundisha leo.

22:20 Mit 8:6Je, sijakuandikia misemo thelathini,

misemo ya mashauri na maarifa,

22:21 1Pet 3:15; Mhu 12:10kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika,

ili uweze kutoa majibu sahihi

kwake yeye aliyekutuma?

22:22 Law 25:17; Zek 7:10; Kut 23:6; Mal 3:5Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini,

wala kumdhulumu mhitaji mahakamani,

22:23 Ay 29:16; Za 12:5; 1Sam 25:39kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao

naye atawateka wao waliowateka.

Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira ya haraka,

usishirikiane na yule aliye mwepesi kukasirika,

22:25 1Kor 15:33la sivyo utajifunza njia zake

na kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.

22:26 Kum 19:14; Mit 23:10Usiwe mwenye kupana mikono katika rehani,

au kuweka dhamana kwa ajili ya madeni.

22:27 Mit 11:15; 17:18Kama ukikosa njia ya kulipa,

kitanda chako

kitachukuliwa ukiwa umekilalia.

Read More of Mithali 22