Mithali 21:5-16 NEN

Mithali 21:5-16

21:5 Mit 10:4Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida,

kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.

21:6 Mit 10:2; 2Pet 2:3Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo

ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.

21:7 Mit 11:5Jeuri ya waovu itawaburuta mbali,

kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa.

21:8 Mit 2:15Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu,

bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu.

21:9 Mit 21:19; 19:13; 25:24Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,

kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.

21:10 Yak 4:5Mtu mwovu hutamani sana ubaya,

jirani yake hapati huruma kutoka kwake.

21:11 Mit 19:25Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa,

mjinga hupata hekima;

wakati mtu mwenye hekima afundishwapo,

hupata maarifa.

21:12 1Kor 10:10; Rum 2:8; Mit 14:11Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu,

naye atawaangamiza waovu.

21:13 Ay 29:12; Zek 7:11; Mdo 7:57; Yak 2:13Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini,

yeye pia atalia, wala hatajibiwa.

21:14 Mwa 32:20; Mit 18:16Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira

na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali.

21:15 Mit 21:9Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki,

bali kitisho kwa watenda mabaya.

21:16 Za 49:14; Eze 18:24Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu,

hupumzika katika kundi la waliokufa.

Read More of Mithali 21