Mithali 21:27-31
21:27 1Fal 14:24; Amo 5:22; Mit 15:8Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo,
si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya!
21:28 Isa 29:21; Mit 19:5Shahidi wa uongo ataangamia,
bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.
21:29 Mit 14:8Mtu mwovu ana uso wa ushupavu,
bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.
21:30 Ay 12:13; Yer 9:23; 2Nya 13:12; Mdo 5:39Hakuna hekima, wala akili, wala mpango
unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.
21:31 Isa 31:1; Za 3:8Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita,
bali ushindi huwa kwa Bwana.
Mithali 22:1-6
22:1 Mhu 7:1Heri kuchagua jina jema kuliko utajiri mwingi,
kuheshimiwa ni bora kuliko fedha au dhahabu.
22:2 Ay 31:15; Mt 5:45; Za 49:1-2Tajiri na maskini wanafanana kwa hili:
Bwana ni Muumba wao wote.
22:3 Mit 14:16; 27:12; Isa 26:20Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,
bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa.
22:4 Mit 15:33; 10:27; Dan 4:36Unyenyekevu na kumcha Bwana
huleta utajiri, heshima na uzima.
22:5 Mit 15:19; 1Yn 5:18Katika mapito ya waovu kuna miiba na mitego,
bali yeye ailindaye nafsi yake hukaa mbali nayo.
22:6 Efe 6:4Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.