Mithali 21:17-26 NEN

Mithali 21:17-26

21:17 Mit 23:20-21, 29-35Mtu apendaye anasa atakuwa maskini,

yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.

21:18 Isa 43:3-4; Mit 11:8Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki,

nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.

21:19 Mit 21:9Ni afadhali kuishi jangwani

kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.

21:20 Za 112:3; Mit 10:22; Mt 25:3Katika nyumba ya mwenye hekima

kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta,

lakini mtu mpumbavu

hutafuna vyote alivyo navyo.

21:21 1Kor 15:58; Za 25:13; Mt 5:6Yeye afuatiaye haki na upendo

hupata uzima, mafanikio na heshima.

21:22 Mit 8:14; Mhu 9:15-16Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu,

na kuangusha ngome wanazozitegemea.

21:23 Za 34:13; Yak 3:2; Mit 12:13Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake

hujilinda na maafa.

21:24 Yer 43:2Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake;

hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.

21:25 Mit 13:4Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake,

kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.

21:26 Law 25:35; Mt 5:42Mchana kutwa hutamani zaidi,

lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.

Read More of Mithali 21