Mithali 20:5-14
20:5 Za 18:16Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina,
lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.
20:6 Za 12:1; Mt 6:2; Mhu 7:28; Lk 18:8Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,
bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?
20:7 Za 26:1; 37:25-26; 112:2Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,
wamebarikiwa watoto wake baada yake.
20:8 1Fal 7:7; Mit 25:4-5Wakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu,
hupepeta ubaya wote kwa macho yake.
20:9 Mhu 7:20; 1Fal 8:46; 1Yn 1:8Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi;
mimi ni safi na sina dhambi?”
20:10 Mit 20:23; 11:1Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti,
Bwana huchukia vyote viwili.
20:11 Za 39:1; Mt 7:16Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,
kama tabia yake ni safi na adili.
20:12 Kut 4:11; Rum 11:26; Za 94:9Masikio yasikiayo na macho yaonayo,
Bwana ndiye alivifanya vyote viwili.
20:13 Mit 6:11; 19:15; Rum 12:11Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,
uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
“Haifai, haifai!” asema mnunuzi,
kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.