Mithali 20:25-30
20:25 Mhu 5:2-5; Yer 44:25Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka
na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.
20:26 Mit 20:8Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu,
hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
20:27 Za 119:105; Mit 16:2Taa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu,
huchunguza utu wake wa ndani.
20:28 Mit 29:14; Isa 16:5Upendo na uaminifu humweka mfalme salama,
kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama.
20:29 Mit 16:31Utukufu wa vijana ni nguvu zao,
mvi ni fahari ya uzee.
20:30 Za 51:2; Mit 22:15Mapigo na majeraha huusafisha ubaya,
nayo michapo hutakasa utu wa ndani.
Mithali 21:1-4
21:1 Es 5:1; Yer 39:11-12Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana;
huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.
21:2 Mit 24:12; Lk 16:15; Yer 17:10; 1Sam 16:7Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,
bali Bwana huupima moyo.
21:3 Hos 6:6; Mik 6:6-8Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika
zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.
21:4 Ay 41:34; Mit 6:17Macho ya kudharau na moyo wa kiburi,
ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!