Mithali 20:15-24 NEN

Mithali 20:15-24

20:15 Ay 28:12, 16, 17, 18, 19Dhahabu kunayo, na marijani kwa wingi,

lakini midomo inenayo maarifa

ni kito cha thamani kilicho adimu.

20:16 Kut 22:26; Mit 27:13Chukua vazi la yule awekaye dhamana

kwa ajili ya mgeni;

lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo

kwa ajili ya mwanamke mpotovu.

Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,

bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.

20:18 Mit 11:14; 24:6Fanya mipango kwa kutafuta mashauri,

ukipigana vita, tafuta maelekezo.

20:19 Mit 11:13Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,

kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.

20:20 Kut 21:17; Mit 30:11; Ay 18:5; Law 20:9Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,

taa yake itazimwa katika giza nene.

20:21 Mit 28:8; Hab 2:6Urithi upatikanao haraka mwanzoni,

hautabarikiwa mwishoni.

20:22 Mit 24:29; Yer 42:11; Kum 32:35; Rum 12:17-19Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!”

Mngojee Bwana, naye atakuokoa.

20:23 Kum 25:13Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu,

nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.

20:24 Mit 19:21; Yer 10:23; Rum 8:26Hatua za mtu huongozwa na Bwana.

Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?

Read More of Mithali 20