Mithali 2:1-11 NEN

Mithali 2:1-11

Faida Za Hekima

2:1 Mit 1:8Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu

na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,

2:2 Mit 22:17kutega sikio lako kwenye hekima

na kuweka moyo wako katika ufahamu,

2:3 Yak 1:5na kama ukiita busara

na kuita kwa sauti ufahamu,

2:4 Ay 3:21; Mt 13:44; 6:19-21na kama utaitafuta kama fedha

na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,

2:5 Kum 4:6ndipo utakapoelewa kumcha Bwana

na kupata maarifa ya Mungu.

2:6 Ay 12:13; Lk 21:15; Yak 1:5Kwa maana Bwana hutoa hekima,

na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

2:7 Mwa 6:9; 15:1; Mit 30:5-6; Za 84:11Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,

yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

2:8 1Sam 2:9; Za 18:25kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki

na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.

2:9 Kum 1:16Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki

na sawa: yaani kila njia nzuri.

2:10 Mit 14:33Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako,

nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.

2:11 Mit 4:6Busara itakuhifadhi

na ufahamu utakulinda.

Read More of Mithali 2