Mithali 19:3-12
19:3 Mit 14:1; 9:13; 24:9; Isa 32:6; Yak 1:13-15Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake
hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana.
19:4 Mit 19:7; 14:20Mali huleta marafiki wengi,
bali rafiki wa mtu maskini humwacha.
19:5 Kut 23:1; Kum 19:19; Mit 1:28Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo hataachwa huru.
19:6 Mit 29:26; 17:8; 18:16Wengi hujipendekeza kwa mtawala
na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.
19:7 Mit 10:15Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote:
Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani!
Ingawa huwafuata kwa kuwasihi,
hawapatikani popote.
19:8 Mit 16:20Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe,
yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.
19:9 Kum 19:19Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa,
naye amwagaye uongo ataangamia.
19:10 Mit 26:1; 30:21-23; Mhu 10:5-7Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa,
itakuwa vibaya kiasi gani
kwa mtumwa kuwatawala wakuu.
19:11 2Fal 5:12; Mit 16:32; Mt 25:21; Efe 4:32Hekima ya mtu humpa uvumilivu,
ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.
19:12 Za 33:3; 72:5-6; Es 1:12Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba,
bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.