Mithali 19:23-29
19:23 Za 25:13; 1Tim 4:8; Ay 4:7; Mit 10:27Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima,
kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,
bila kuguswa na shida.
19:24 Mit 26:15Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!
19:25 Za 141:5; Mit 9:9; 21:11Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara,
mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa.
19:26 Mit 28:24Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake
ni mwana aletaye aibu na fedheha.
19:27 Mt 7:15; Mk 4:24; Efe 4:14Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho,
utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.
19:28 Ay 15:16Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu
na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi.
19:29 Kum 25:2; Mit 26:3Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka
na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.
Mithali 20:1-4
20:1 Law 10:9; Hab 2:5; 1Sam 25:36; 1Fal 20:16; Mit 31:4Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi;
yeyote apotoshwaye navyo hana hekima.
20:2 Mit 8:36; 19:12; Es 7:7Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;
yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.
20:3 Mwa 13:8; Mit 17:14Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi,
bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.
20:4 Mit 6:6; Mhu 10:18Mvivu halimi kwa majira;
kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama
lakini hapati chochote.