Mithali 19:13-22 NEN

Mithali 19:13-22

19:13 Mit 10:1; Es 1:18; Mit 21:9Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye,

naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.

19:14 2Kor 12:14; Mit 18:22Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi,

bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

19:15 Mit 10:4; 20:13Uvivu huleta usingizi mzito,

naye mtu mzembe huona njaa.

19:16 Mit 16:17; Lk 10:28; Rum 2:7Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake,

bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.

19:17 Kum 24:19; Mt 10:42; 2Kor 9:6Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana,

naye atamtuza kwa aliyotenda.

19:18 Mit 13:24; 23:13-14Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini,

usiwe mshirika katika mauti yake.

Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake,

kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena.

19:20 Mit 4:1; 12:15Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho,

nawe mwishoni utakuwa na hekima.

19:21 Es 9:25; Mhu 7:29; Yer 4:29; Mao 3:37; Ebr 6:17Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,

lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.

Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,

afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.

Read More of Mithali 19