Mithali 18:7-16
18:7 Za 140:9; 64:8; Mhu 10:12Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake
na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.
18:8 Mit 26:22Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;
huingia sehemu za ndani sana za mtu.
18:9 Mit 28:24Mtu aliye mlegevu katika kazi yake
ni ndugu na yule anayeharibu.
18:10 2Sam 22:3; Za 61:3; 18:2Jina la Bwana ni ngome imara,
wenye haki huikimbilia na kuwa salama.
18:11 Mit 10:15Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,
wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.
18:12 Mit 11:2; 15:33Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,
bali unyenyekevu hutangulia heshima.
18:13 Mit 20:25; Yn 7:51Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza,
huo ni upumbavu wake na aibu yake.
18:14 Mit 15:13; 17:22Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa
bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?
18:15 Mit 15:14; Efe 1:17Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa,
masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
18:16 Mwa 32:20; 39:2-6; 41:38-44; 1Sam 10:4Zawadi humfungulia njia mtoaji,
nayo humleta mbele ya wakuu.